SOKA LINAVYOWEZA KUMNUFAISHA MTOTO WA KIKE
NA MARYAM NASSOR, ZANZIBAR
SOKA ndio mchezo maarufu zaidi
duniani, hakika ni mchezo unaofuatiliwa zaidi kwenye sayari hii, kutokana
na mvuto wake wa kimataifa.
Wanasoka
ndio watu wenye umaarufu mkubwa, kutokana na kuwa na majina makubwa.
Ni Kweli, kwa hapa Zanzibar ukizungumzia soka
la wanawake huwezi kuacha kulitaja jina la
Binasra.
Ni mkufunzi
ambae anatambulika na shirikisho la mpira wa miguu la Afrika (CAF)na lile la kimataifa (FIFA).
Pia amesoma na kupata leseni yenye gredi ‘A’ kwa Tanzania ni
mwanamke pekee, na kwa wachezaji wa
Zanzibar ni hazina ambayo wanatakiwa wachezaji wakike kuitumia.
Akizungumza
na mwandishi wa makala haya, katibu wa chama cha mpira wa wanawake Zanzibar
Neema Machano Othman, anasema mpira wa timu za wanawake umekuwa ukilinganisha
na hapo awali.
Kwa hapa Zanzibar, kuna walimu wazuri ambao
wanajulikana kimataifa, hivyo ni rahisi kwa wachezaji kujifunza na kufikia ndoto zao za kimichezo.
‘’ Hapa
kwetu Zanzibar soka la wanawake, limekuwa ukilinganisha na hapo awali miaka
mitano iliyopita tulianza na timu tatu tu ‘’alisema.
Aidha alisema kuwa, Lakini kwa sasa wamefika hadi timu kumi, ambazo unguja ziko nane na
Pemba ziko mbili.
Saada Saidi
mchezaji wa timu ya wanawake ya
warrious, alisema soka la Zanzibar linakuwa na wanamalengo makubawa ya kimichezo lakini tatizo kubwa ni
ufadhili katika ligi ya wanawake.
Alisema
kuwa, ligi ya wanawake bado inasuwa suwa ukilinganisha na ligi ya wanaume,
kutokana na kuwa bado soka la wanawake halijaaminika hapa Zanzibar , kama kule
Tanzania bara.
“ Kule kwa
wenzetu bara , ligi ya wanawake inapata wadhamini wa kuidhamini ligi na
wachezaji wanafikia ndoto zao, kama oppa clement ambae anachezea timu ya misri na mshahara wake
ni mkubwa” alisema.
Aidha
aliwataka wadhamini kujitokeza kuidhamini ligi ya wanawake hapa Zanzibar, kwani
ligi imesimama kutokana na kukosekana kwa mdhamini.
Hafidha Juma
Ali, ni mchezaji wa timu ya New Generation ya wanawake, anasema michezo
ni afya pia nia ajira, lakini Serikali kama mdau nambari moja ije na
mipango endelevu ya kuinua na kuihamisha ili iwe ajira kwa vijana.
Alisema kuwa, soka la wanawake bado linakabiliwa na changamoto lukuki hasa kwenye udhamini, hivyo serikali idhidi kuweka mazingira mazuri na kuwatafutia mdhamini kutokana na kuwa wao ndio wanaanza hawajaaminika na wafadhili.
“ Tunahamu
na sisi wachezaji kutoka Zanzibar tucheze timu kubwa za kulipwa , na ari na
moyo wa kujituma tunao, lakini bado soka
la hapa kwetu linasua sua’’ alisema.
Juma Mohamed
Juma kocha wa timu ya wanaume mwembeladu sc, anasema soka la wanawake linakuja
vizuri kwa sasa kutokana na hapo awali lilikuwa halina hamasa.
Alisema
kuwa, wachezaji wa kike wasikate tamaa kutokana na vikwazo vilivyopo na
kupambana kuonesha uwezo wao, kwani’ hata mbuyu ulianza kama mchicha’.
Hivyo, aliwataka wapambane kujituma kwani
mpira wa wanawake na wanaume uko tofauti, na hata hapo zamani ligi ya wanaume
ilikuwa haina mdhamini, lakini baada ya kupambana wamefanikiwa kuupata
udhamini.
Nae katibu
wa shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar ( ZFF) Hassan Ahmada Vuai alipokuwa
akizungumza na mwandishi wa makala haya alikiri kuwa ligi ya soka la wanawake
imesimama kutokana na kuwa haina udhamini.
Alisema
kuwa, bado hawajapata wadhamini wakuiidhamini
ligi ya wanawake, hivyo wanaziomba taasisi binafsi kujitokeza kuidhamini ligi
hiyo.
Aidha
alisema kuwa, ligi ya wanawake imekosa
sapoti kutokana na kuwa jamii bado hawajataka kubadili mitazamo yao, na kuona
mwanamke popote anaposhiriki basi anafanikiwa mfano mzuri niRaisi wa jamuhuri
wa Tanzania anavyosonga mbele.
Hija Mohamed
Ramadhani, mshauri wa maswala ya jinsia katika michezo kutoka shirika la
Ujerumani (G IZ)hivi karibuni alipokutana na wandishi wa habari, alisema mradi
wa michezo kwa maendeleo hapa Zanzibar
utaboresha mazingira mazuri ya mindombinu ya viwanja na inalengo la
kujenga viwanja saba Unguja vinne na Pemba vitatu .
Lakini ipo
haja kwa shirika hilo na taasisi nyengine kujitoa zaidi kudhamini ligi za timu
za wanawake ili kuwapa hamasa na kuiona hasa ile dhana ya michezo kwa maendeleo
inavyofanya kazi kwani waswahili wanasema ‘ kuona ndio kuaminii’.
MWISHO
Post a Comment