SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR BADO KITENDAWILI.
NA MARYAM NASSOR,
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa
kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa sheria mpya ya habari kutokana na kuwa
bado ni kitendawili.
Akizungumza
katika kikao cha majadiliano ya sheria kandamizi za
habari , katika ofisi kuu ya TAMWA ZNZ , huko Tunguu Unguja mjumbe wa
bodi hiyo Bi Hawra Shamte alisema bado
kuna utata mkubwa kuhusu sheria hiyo.
Alisema,
kiukweli hiyo sheria haijulikani
imefikia hatua gani na iko wapi kwasasa, kutokana na kuwa kila mmoja anasema la
kwake.
“ Tulitegemea
siku ya uhuru wa habari tungeambiwa kuhusu sheria hiyo kuwa, imefikia wapi au lini itazinduliwa lakini bado hatujui hatua iliyofikiwa”,
Alisema.
Aidha,
aliwataka wandishi wa habari kuendelea kufanya uchechemuzi juu ya upatikanaji
wa sheria mpya ya habari nchini.
Mratibu wa baraza la habari Tanzania kwa
upande wa Zanzibar,Bishifaa said Hassan alisema kuwa, waandishi waendelee
kupaza sauti zao kudai sheria mpya ya
habari.
Alisema kuwa,kutokana na kuwepo haja ya sheria
rafiki kwa wandishi, hali hiyo imezidi kwasasa kutokana na kuwa wandishi wahabari wanakosa
uhuru wa kujieleza, hata katika siku ya uhuru wa habari.
“ Hii hali ni mbaya kwasasa wandishi wa habari
wanakosa uhuru wa kujieleza hata katika siku ya uhuru wa habari, wakajieleze wapi’’
alisema.
Nae, Salum Said
ambae ni mwandishi wa habari mkongwe , alisema kuwa sheria zilizopo
haziumizi tu, uhuru wa habari bali
zinawaumiza wananchi kwa ujumla.
Alisema kuwa,
uhuru wa habari hauwezi kupatikana
endapo kutakuwa na sheria kandamizi ambazo zinawakandamiza wandishi na wananchi.
Aidha, aliwasihi wandishi wa habari nchini kuendelea
kufanya ufuatiliaji ili sheria mpya ya habari ipatikane kutokana na kuwa
ni zaidi ya miaka 20 sasa wamekuwa
wakiifuatilia sheria hiyo.
Wakichangia katika kikao hicho, baadhi ya waandishi wa habari walisema kuwa.
Wamekuwa wakikutana na vikwazo vingi
katika kufanikisha majukumu yao, hali
inayowasababishia kukosa uhuru na kuwajibika ipasavyo.
Kikao hicho cha siku moja, kimeandaliwa na TAMWA
ZNZ kwa wandishi na wadau wa habari kwa lengo la kuendelea kufanya ufuatiliaji
wa sheria mpya za habari nchini.
MWISHO
Post a Comment