WANDISHI WA HABARI KUHAMASISHA USAWA WA KIJINSIA MICHEZONI
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuhamasisha wauguzi wa
kike kuingia katika kada ya uguuzi na tiba michezoni ili iwe hamasa kwa watoto
wa kike kushiriki katika soka.
Akizungumza katika mafunzo ya siku tano ya
wandishi wa habari za michezo huko
ofisi ya TAMWA ZNZ, Tunguu Unguja, mwandishi
na mhariri wa habari za michezo kutoka gazeti la Zanzibar leo, Salum Vuai.
Alisema, kumekuwa na uchache wa wauguzi wa kike katika michezo, au katika timu
nyengine hakuna kabisa kwa hapa Zanzibar.
“ Kama munataka wanawake wengi
kushirikia katika michezo, basi ni vizuri kwanza muwahamasishe wauguzi wakike
kuingia katika tasnia ya michezo ili wawastiri wenzao wanapopatwa na shida
viwanjani’’ alisemAa
Aidha aliishauri Serikali kurejesha ruzuku katika vyama vya
michezo ili isaidie kuajiri wauguzi hao, kutokana na kuwa timu nyingi za
wanawake ni maskini hivyo ni vigumu kutekeleza hayo.
Nae, mkufunzi katika mafuzo
hayo Bi hawra Shamte aliiwataka wandishi wa habari kuhamasisha wanawake
kushiriki katika michezo kwa maendeleo kutokana na kuwa michezo ni ajira .
" Siku hizi mpira ni ajira , tumekuwa tukisika timu za kiume wachezaji wananunuliwa kwa bei ghali hivyo, wanaweza kujiajiri kupitia michezo kwa kutumia dhana ya michezo kwa maendeleo,"alisema.
Alisema kuwa, licha ya kuwepo katiba na sera ya michezo ya mwaka 2018 lakini
bado kuna ushirikishwaji mdogo wa usawa wa kijinsia katika michezo. Hivyo,
aliwataka wandishi wa habari kuihamasisha jamii katika ngazi ya familia, ili
wazazi waruhusu na kusaidia wasichana kushiriki katika michezo
. Nao, baadhi ya
washiriki katika mafunzo hayo, waliahidi kufanya kazi kwa bidii ya kuihamasisha
jamii ili kuruhusu wasishana na wanawake kushiriki katika michezo kama haki yao
ya msingi ya kikatiba.
Programu ya michezo kwa maendeleo, inatekelezwa na TAMWA
ZNZ, ZAFELA na Cente for Youth Dialogue kwa kushirikiana na Deuth Gesellschaft
fur intetnational Zusammenrbeit (GIZ) shirika la Ujerumani ikiwa na lengo la
kuhamasisha waandishi wa habari kuandika bahari za michezo na ushirikia wa
wanawake katika michezo.
MWISHO



Post a Comment