MTUHUMIWA WA KESI YA KUBAKA NA KUTOROSHA ACHILIWA HURU
NA MARYAM NASSOR
MAHAKAMA maalum ya
kupinga udhalilishaji , mkoa wa Kaskazini Unguja , imemuachia huru kijana
Tamimu Ame Juma(28)wa Mahonda Karachi
kwa madai ya kuwa ushahidi uliyoletwa mahakamani hapo haukumtia hatiani.
Akisoma Uwamuzi
mdogo,(Ruling) hakimu wa Mahakama hiyo Lusiano Makoe Nyengo alisema kuwa katika kesi
hiyo mahakama ilisikiliza mashahidi watatu na kielelezo kimoja.
Alisema kuwa, katika
mashahidi wote hao , hakuna ushahidi Mzuri ambao unaweza kumtia
hatiani mtuhumiwa huyo moja kwa moja Hivyo,anamuwachia huru chini ya kifungu cha
215 cha Mwaka 2018.
Alisema kuwa, mshitakiwa
huyo ,alishtakiwa kwa makosa Mawili , kosa la kwanza lilikuwa ni kutorosha na la pili ni kubaka lakini , muhanga alipokuwa
anatoa ushahidi wake, Hakusema ni lini na wapi aliingiliwa na
mtuhumiwa huyo.
Aidha alisema kuwa, ushahidi mzuri ni wa muhanga na mahakama
inauzingatia lakini shahidi namba mbili alikuwa ni muhanga, alipokuja mahkamani
alisema ni kweli kabakwa, lakini
hakuweza kuieleza mahkama kuwa kabakwa eneo gani na ilikuwa lini.
Hakimu
Lusiano, alisema kuwa baada ya kuuangalia ushahidi huo, mahakama ilijielekeza
katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ni umri na kuingiliwa, jee muhanga aliingiliwa
kweli na mtuhumiwa, shahidi daktari alipokuja mbele ya Mahakama alisema kuwa ,
alipompima alimkuta yuko kwenye siku
zake hivyo alishindwa kusema kuwa mtoto kaingiliwa au laa.
Alisema, na kuhusu umri muhanga hakusema kuwa yeye ana miaka
mingapi , na shahidi namba moja alikuwa ni mama yake na yeye hakusema pia kuwa mwanawe ana miaka mingapi.
Alisema kuwa, mpelelezi alipokuja mahakamani alisema , Muhanga alibakwa kama alivyoambiwa na muhanga mwenyewe wakati ana muhoji, lakini hakueleza mazingira gani muathirika alibakwa.
Hakimu huyo, alisema
kuwa na kosa la pili lilikuwa ni kubaka, lakini pia ushahidi haujitoshelezi
ambao hauoneshi, Mtoto ni kwa namna gani alivyobakwa.
“Kwa mantiki hiyo, ushahidi uliyokuwepo mbele ya mahakama hii, hauoneshi kuwa mtuhumiwa ana kosa la kujibu na badala yake inamuachia huru” alisema.
. Mshtakiwa huyo, Tamimu Ame Jecha, alishtakiwa kwa makosa mawili, la kwanza likiwa ni kutorosha msichana aliye chini ya uwangalizi wa wazazi wake kinyume na kifungu 113 (1) (a) cha sheria za adhabu namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar, na kosa la pili ni kubaka kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na 109 (1) ya sheria ya makosa na adhabu namba 6 ya mwaka 2018 sheria za Zanzibar.
Awali mshtakiwa huyo, Ilidaiwa Mahkamani hapo kuwa siku ya tarehe 25/01/2024 majira ya saa 11 za jioni huko Mahonda
Karachi , Wilaya ya Kaskazini ''B'' Unguja
bila ya halali alimchukua mtoto wa kike Mwenye Umri wa Miaka 16 ambae hajaolewa na aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake,
kutoka Posta Mahonda na kumpeleka nyumbani kwake. Bila ya ridhaa ya wazazi wake
jambo ambalo ni kosa kisheria.
MWISHO


Post a Comment