HAKIMU KASKAZINI UNGUJA, AZINDUA MUONGOZO WA JAJI MKUU ZNZ
NA MARYAM NASSOR, MAHKAMA ya Mkoa wa kaskazini Unguja imezindua muongozo namba 1/2024 wa Mh.Jaji mkuu wa Zanzibar wa kuweka ukomo wa usikilizaji wa mashauri Mahkamani.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, huko Mahonda, hakimu
dhamana wa Mkoa wa kaskazini Unguja Lusiano Makoe Nyengo, alisema lengo
la muongozo huo wa Jaji mkuu wa Zanzibar ni kuhakikisha kuwa, mashauri yote yanayofika Mahkamani yanamazilizika kwa
wakati na haki inapatikana kwa wananchi.
Aidha,
aliwasisitiza wananchi wa Mkoa wa Kaskazini kuiunga mkono Mahkama kwa kuhakikisha wanakwenda Mahkamani
kutoa ushahidi ili lengo la Mheshimiwa Jaji Mkuu la kuona kesi zinaendeshwa
kwa haraka linafikiwa.
Akieleza, muongozo huo, lusiano alisema kwa Mahkama za mikoa mashauri ya jinai yasizidi miezi 12 yawe yamemalizika, toka siku ya kwanza kufunguliwa.
Alisema kwa upande wa Mahkama za wilaya mashauri ya madai na jinai yasizidi miezi sita, yawe yamemalizika toka siku ya kwanza kufunguliwa na mahkama za mwanzo mashauri yasizidi miezi mitatu, yawe yamemalizika
Kwa upande
wake, kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Unguja Kamugisha, alisema jeshi la
Polisi litashirikiana na Mahkama kuona
muongozo huo, unatekelezwa kwa
kuhakikisha wanaleta mashahidi Mahkamani na kukamilisha upelelezi,na kesi
zimalizike kwa haraka.
Muendesha
mashtaka dhamana wa Mkoa wa Kaskazini Unguja,Shumbana Mbwana , alisema ili kufanikisha muongozo huo,kunahitajika mashirikiano ya
pamoja baina ya Mahkama, waendesha
mashtaka na mawakili ili kumaliza
kesi kwa haraka.
Uzinduzi wa
muongozo huo, ulifanyika katika Mahkama ya mkoa Mahonda, ambao ulikwenda
sambamba na kikao cha kusukuma mbele mashauri ya jinai.
MWISHO


Post a Comment