TAMWA ZNZ YAKOSA MASHIRIKIANO NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI.


 NA MARYAM NASSOR,

CHAMA cha Wandishi wa habari Wanawake Zanzibar (TAMWA) kimesema  hakina mashirikiano mazuri na baadhi ya vyombo vya habari na kupelekea  kumkosa mshindi wa tunzo za uwandishi  mahiri wa habari  kwa upande wa  runinga.

Akizungumza  katika mkutano na wandishi wa habari mkurugenzi wa Tamwa Zanzibar Dr Mzuri Issa alisema  viwango vya uweledi katika uwandishi vimeshuka kutokana na kusekana kwa mashirikiano  mazuri kwa baadhi ya vyombo hivyo.

Alisema, ukiangalia wandishi wengi waliyopata tunzo  hizi ,walikuwa na mashirikiano nao na wamiliki wa vyombo vyao , hivyo inakuwa rahisi kwao kushirikiana katika mafunzo kabla ya mashindano.

“Baadhi ya  wamiliki wa vyombo vya habari hatupati mashirikiano nao kwani hata tukiwaita kwenye semina tuje kuwapa mafunzo hawaji au wanawaleta wandishi wadogo, hivyo hata ule mrejesho nahs hawaupati” alisema.

Aidha , Dr mzuri alisema kuwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika mashindano hayo, lakini wanawapongeza wandishi wa habari kwa kushiriki kwa wingi, kwani kwa mara hii kazi ziliongezeka hadi kufikia 529, inaonesha ku wa wandishi wamepata hamasa.

Nae, Jaji katika mashindano hayo Dr Abdullah Mohamed Juma akizungumza kwa niaba ya majaji wenzake alisema kuwa kazi hiyo, wameifanya kwa uweledi mkubwa, na kama kuna mapungufu basi madogo madogo yaliyojitokeza ni ya kibinadamu tu.

Alisema, mashindano ya mwaka huu yamemurika  nafasi ya mwanamke katika jamii, ushiriki wa makundi umeongezeka kwa idadi na ongezeko kubwa la wandishi wanawake.

Alisema kuwa,makala zilizoletwa zilikuwa na ubora na zilionesha nafasi ya mwanamke katika uongozi na hilo ndio ilikuwa lengo, na inaonesha mabadiliko chanya yanakuja kwa kasi na siyo pole pole.

“Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na vipengele vingi, lakini lengo kwa kiasi Fulani lilifikiwa kwani wandishi walijitahidi kuonesha changamoto za wanawake katika nafasi za uongozi” alisema.

Nae, Binasra Mohamed Juma  Jaji katika mashindano hayo, alisema moja ya changamoto aliyoiona katika mashindano hayo ni wandishi wengi hawafanyi kazi kwa viwango vinavyotakiwa.

Salum Vuai, mwandishi kutoka  gazeti la Zanzibar leo, alisema kuwa wandishi wengi wa siku hizi hawana wahariri wenye uzoefu unaotakiwa  kwa baadhi ya vyombo vya habari hivyo, wanakosa wasimamizi wazuri wa kazi zao.

No comments

Powered by Blogger.