MAJAJI WAANZA KAZI RASMI KUCHAMBUA KAZI ZA TUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA TABIACHI ZA '' COMMUNITY FOREST''
NA MWANDISHI WETU,
JOPO la majaji limeanza rasmi kupitia na kuchambua kazi zilizowasilishwa na waandishi wa Habari na vyombo vya habari katika Tuzo ya Uandishi wa Habari za Tabianchi za Community Forests.
Mchakato huu
,ni hatua muhimu kuelekea hafla ya utoaji wa tuzo itakayofanyika tarehe 28
Machi 2026.
Kupitia tuzo
hizo , Meneja wa Mawasiliano kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ ) Bi Sophia Ngalapy amesema Community Forests Pemba, Community Forests International na TAMWA-ZNZ
wanalenga kutambua na kuhamasisha uandishi wa habari unaoangazia mchango na
uongozi wa wanawake katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Zanzibar.
Amesema Majaji hao,
wanapitia kazi mbalimbali zilizowasilishwa kutoka vyombo tofauti vya habari ili
kuhakikisha kuwa kazi zenye ubora na zinazobeba simulizi za mabadiliko chanya
zinapata nafasi ya kutambuliwa katika tuzo hizo.
Jumla ya
kazi 73 zimewasilishwa na waandishi wa habari kutoka katika makundi ya
magazeti, redio, televisheni na mitandao ya kijamii, huku vyombo vya habari 7
kutoka Zanzibar.
Post a Comment