MBUNGE WA CHADEMA ZANZIBAR AJIONDOA CHADEMA NA KUHAMIA CHAMA CHA MAPINDUZI ( CCM)


 

 

Na Maryam Nassor

MUHESHIMIWA Mbunge  Asya Mohamed Muhidini kutoka chama cha  Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  amekihama chama hicho na kuhamia chama cha Mapinduzi ( CCM).

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi,  jana   June , 27 . 2025,  huko  Jijini Dodoma amesema tayari ameshakihama  chama hicho na kuhamia CCM.

 Mbunge Asya amesema,  amehamia Chama Cha Mapinduzi na ametia nia ya kushiriki Uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

" Tayari nimehama  chama cha Mapinduzi CCM na  naahidi kushiriki katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa Oktoba 2025" amesema Mbunge Asya. 


No comments

Powered by Blogger.