Sheria mpya ya Habari Zanzibar Bado kizungumkuti.

 NA MARYAM NASSOR


WIZARA ya Habari  Vijana Utamaduni  na Michezo Zanzibar imesema itahakikisha inaweka mazingira mazuri ili Sheria mpya ya Habari ipatikana.

Ameyasema hayo Mkurugenzi wa Habari Maelezo Zanzibar Salum Ramadhani Hamad, alipokuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, huko katika ukumbi wa Rahaleo  Unguja katika  kilele Cha madhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.

Amesema kuwa, Wizara hiyo  Ina mtazamo wa kuhakikisha  inaweka mazingira mazuri yakiwemo kupatikana sera na Sheria mpya ya Habari.

" Jukumu kubwa nililopewa ni kulimaliza suala la upatikanaji wa Sheria mpya ya Habari na naomba muniamini siahidi ni lini kwa sababu ni mchakato lakini itapatikana " amesema Katibu.

Aidha amesema kuwa,  Wizara hiyo karibuni wanatutegemea kuzindua sera ya Habari  ya mwaka 2024 ambayo  tayari imeshakamilika.

Nae, Mkurugenzi wa Baraza la Habari Tanzania Zanzibar MCT, Ziada Ahmed Kombo amesema ni wajibu wa Serikali kuhakikisha  wanaweka mazingira mazuri  ya wana habari yakiwemo kupatikana Sheria mpya ya Habari.

Amesema kuwa, ni lazima Serikali kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi zao katika Hali ya uhuru na haki na hayo yatapatikana endapo Sheria mpya ya Habari itapatikana.


" Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha waandishi wa habari wanafanya kazi zao katika mazingira mazuri  na hayo yatapatikana endapo tu Sheria mpya na rafiki  ya habari itapatikana " amesema Ziada.

 Nae, mwandishi wa Habari mkongwe Visiwa Zanzibar Salim Said amesema 
Waandishi wa habari Zanzibar wamechoka  kusikia kauli mbali mbali za Serikali juu ya upatikanaji wa Sheria mpya ambazo hazina ukwelii.

"Tumechoka kusikia Sheria mpya Iko mbioni au  hivi karibuni wanategemea kuupeleka kama muswada Baraza la wawakilishi  kauli ambazo hazina ukwelii wowote" anasema bwana Salim.

 Aidha amesema kuwa,  ni Zaidi ya miaka 20 tokea waanze harakati za kudai Sheria mpya na rafiki ya habari Zanzibar bila ya mafanikio yoyote.

 Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar ( TAMWA ZNZ )  Dk Mzuri Issa amesema katika kilele Cha madhimisho hayo, amesema haki  na wajibu siku zote ni watoto pacha.

 Amesema  kama waandishi wa habari wanatakiwa kutimiza wajibu wao basi na Serikali lazima ifanye haki kwa kuwapatia Sheria mpya ya Habari ambayo ni kilio chao Cha muda mrefu.

 Nae, Mjumbe wa  Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar ' WAHAMAZA' Bi Hawra Shamte amesema kuwa waandishi wa habari wa Zanzibar wanatamani  siku Moja Sheria mpya na rafiki ya Habari itapatikana kwani ni kilio  chao Cha siku nyingi.

Katika  kilele Cha madhimisho hayo ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ya mwaka huu,waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari  walishiriki pamoja na wadau wa Habari kauli mbiu ya mwaka huu ni " Sheria nzuri ya Habari ni chachu ya Uchaguzi ulio huru na wa haki"
        Mwisho 

No comments

Powered by Blogger.