WAANDISHI WA HABARI ENDELEENI KUPAZA SAUTI ZA WANAWAKE -TAMWA ZNZ
NA MARYAM NASSOR
WAANDISHI wa Habari wametakiwa kuendelea kuandika Habari za wanawake ambao bado sauti zao hazijasikika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi .
Akizungumza
na wandishi wa Habari , Meneja miradi kutoka Chama cha wandishi wa Habari wanawake Tanzania Zanzibar( TAMWA ZNZ) Nairat
Abdulla huko katika Afisi za chama hicho Tunguu.
Amesema, wanawake wengi wanafanya kazi kubwa
katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kulima na kuhifadhi mikoko lakini jitihada zao hizo
bado hazijaonekana katika jamii.
Amesema kuwa, utafiti uliyofanya na chama hicho umebaini kuwa bado uwepo na ushiriki wao katika shughuli
hizo haujapewa kipaumbele ipasavyo, kupitia vyombo vya habari .
“ Utafiti tuliyofanya TAMWA, ZNZ umegundua bado sauti za wanawake hazijasikia ipasavyo kupitia vyombo vya Habari katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi , hivyo wandishi wanapaswa kuongeza nguvu katika eneo hilo” amesema Nairat.
Nae, Meneja
Mashiriano ya Kimataifa kutoka Jumuiya
ya Kutunza Mazingira ya Kimataifa ( CFI )
Lilian Simule amesema, mradi wa Zanz
Adapt wanahamasisha wakulima
viongozi kutumia vyombo vya Habari
kutangaza kazi zao.
Amesema kuwa, mradi huo unawawezesha wakulima kulima kilimo mseto na kilimo biashara, hivyo ni vyema kujitangaza ili jamii ijuwe wanafanya nini katika kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha kwa
upande wake, Meneja wa Mawasiliano
kutoka TAMWA,ZNZ Sophia Ngalapi alisema waliona kuna umuhimu mkubwa wa kurejea mafunzo hayo kwa wandishi wa Habari
ili kuwaweka sawa.
“ Tumeona
ipo haja kubwa kuyarejea haya mafunzo ili kusikiliza maoni yenu na kukumbushana
maeneo ya mradi huu ili musiende kinyume” alisema Ngalapi.
Nae, Afisa Kilimo Msitu Rhoda Daniel Kadaso alisema mradi huo umeanzisha vitalu vya miche ya misitu na mboga mboga kwa lengo la kuwasaidia wakulima wa mradi huo, kupata miche bora na kwa wakati ili kuongeza kipato chao.
“ tuliwatowa wakulima wa mazao kutoka hapa Zanzibar Kwenda Tanzania bara ili kupata uzoefu na kujifunza kilimo zaidi na kuona jinsi gani wenzao wanalima na kupata
faida”
Nae,
Afisa Mawasiliano kutoka Jumuiya ya
kuhifadhi Misitu Pemba ( CFP) Munira Kaoneka amesema katika mradi huo wanataka wandishi wa
habari kuandika zaidi katika
kuwahamasisha wanawake kuona umuhimu wa kumiliki ardhi .
Amesema kuwa, wanawake wengi hawamiliki ardhi hasa
huko vijijini ,na wanaomiliki hawana hati za umiliki wa ardhi kisheria .
“ Tunataka wandishi wahamasishe wanawake waone
umuhimu wa kumiliki ardhi lakini pia wawe na hati za umiliki kisheria ili ”
amesema Munira.
Mafunzo hayo, ya siku tatu yameandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari
Tanzania Zanzibar( TAMWA ZNZ,) Jumuiya
ya Kuhifadhi Misitu Pemba ( CFP) na
Jumuiya ya Kuhifadhi Mazingira Kimataifa ( CFI) na kuwashirikisha wandishi 20 waliyokuwemo
katika mradi huo.
Mwisho






Post a Comment