Kwanini mkataba wa ulinzi kati ya Pakistan na Saudi Arabia unaitia India wasiwasi


Wiki iliyopita, Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, alipokutana na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, mjini Riyadh, walikumbatiana kwa ishara ya mshikamano.

Mkutano huo ulifanyika mara tu baada ya mataifa hayo mawili kusaini mkataba wa kimkakati wa ulinzi wa pamoja – hatua inayozidi kuikaribisha Pakistan, nchi pekee ya Kiislamu yenye silaha za nyuklia, kwa Saudi Arabia, taifa lenye nguvu kubwa kwenye eneo la Ghuba.

Afisa mmoja mwandamizi wa Saudi Arabia aliieleza Reuters kuwa ''mkataba huu ni njia ya kurasimisha ushirikiano wa muda mrefu uliokuwepo.''

Lakini kwa upande wa India, hali ni tofauti, wengi wanauona kama tishio.


 

No comments

Powered by Blogger.